Monday, 2 March 2020

RED BUTTERFLY - 4

RED BUTTERFLY - 4
RED BUTTERFLY - 4


Yule mwanamke akamnyanyua kwa nguvu Christopher kwa kutumia mkono wa kulia, sasa walikuwa wamesimama sambamba. Meneja Christopher mbele, yule Mwanamke wa mwenye kasi ya ajabu na shabsha ambaye walikuwa wanamtambua kwa jina la Red butterfly alikuwa nyuma.

"Niseme tena tu uhai wa huyu fala ninao mimi. Hata mkinipiga risasi roho yangu haitoenda motoni kabla sijaichakaza vibaya san shingo ya huyu mjinga. Sasa ombi ni moja tu kwenu, wekeni silaha chini na mnipishe hapo mlangoni. La sivyo nitakufa lakini nitakuwa nimeuwa..." Yule mwanamke alisema kwa kujiamini na woga wote uliomvaa awali ulikuwa umemtoka. Alijua ile ni karata yake pekee ambayo ilimpasa kuitumia vizuri kujiokoa. Maneno aliyoyasema yaliingia vizuri kwa wale askari. Na walijua kwamba mwanamke alikuwa anasema kweli. Alikuwa na uwezo wa kuuwa kabla hajafa. Na dhamira yao kama askari ilikuwa kumlinda meneja Christopher na sio kusababisha kifo chake. Ilikuwa dhima kuu ya askari, kulinda raia.

"Nakuuwaaa mwanaume.." Yule mwanamke alisema kwa sauti ndogo sikioni mwa meneja Christopher.

"Jamani naombeni mnisaidie ataniua huyu..." Meneja Christopher alikuwa anasema huku analia. Aliruhusu mkojo kumtoka mtoto wa kiume.

"We komaa! Sio wakusaidie, wapishe mlangoni tuondoke zetu.." Yule mwanamke alisema kwa ukali.

"Adrian. Nahesabu hadi tatu. Kama hamthamini uhai wa huyu raia mwema kwa sababu ya kunikamata mimi basi sawa" Yule mwanamke aliacha hiyo sentensi iingie kwa wale askari kisha akaanza kuhesabu.

"Moja, Mbi..." Hakumaliza mbili. Askari wote sita wakiongozwa na Adrian waliweka silaha chini. Hawakutaka kuwa sababu ya kifo cha yule raia mwema. Kwa maana yule mwanamke alikuwa anamaanisha, sura na sauti yake zilikuwa shahidi.

"Natoka nje na huyu mwanamme. Silaha yangu itahitaji mguso mdogo sana kuitoa risasi katika chemba na kuitoa roho ya huyu mjinga. Ninachomaanisha sitaki yeyote yule alete ujanja ( akatukana tusi kubwa la nguoni). Kwanza nyote sogeeni kuleee" Yule mwanamke alisema huku akiionesha kona moja pembeni ya ile ofisi. Na wale askari walitii. Yule mwanamke alikuwa ameushika usukani sasa kwa kujiamini.

Yule mwanamke akaanza kumkokota meneja Christopher kwa tahadhari kubwa sana. Mkongojo sasa ukielekezwa kwa zamu kwa wale askari. Akapita naye mlangoni kwa kasi na kutoka nje. Akauvuta ule mlango wa ofisi na kuufunga kwa nje. Akamsukuma yule meneja mlangoni na kukimbilia kwenye pikipiki yake nyuma ya ile ofisi. Aliwasha na kutokomea kwa kasi akiwaacha wakina Adrian wamezubaa ofisini. Ni meneja Christopher ndiye aliyewafungulia mlango dakika tatu baadae baada ya kujitambua. Red butterfly alikuwa ametokomea...

***SURA YA NNE***

Baada ya nusu saa Adrian Kaanan alikuwa pembeni ya kitanda cha Daniel Mwaseba katika hospitali ya Kairuki. Alikuwa amemwelezea kila kitu kilichotokea kule katika kiwanda cha nguo cha Urafiki. Daniel alimwelewa Adrian lakini alikuwa hajamwelewa kabisa.

"Kwanini unahisi huyo mwanamke ni Red butterfly, wakati Red butterfly tunaamini ni mzee au hujivika umbo la kizee. Sasa huyo aliyewafungia nyie katika ofisi ya meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki mnasema alikuwa ni msichana mrembo?" Daniel Mwaseba alimuuliza Adrian.

" Mimi naamini yule mwanamke ndiye Red butterfly. Wepesi na kasi ulionielezea ni ileile nilioushuhudia kwa macho yangu. Hata Idd amethibitisha yule ni Red butterfly. Alikuwa anajivika tu umbo la bibi kizee, lakini kwa meneja alikwenda kwa umbo lake halisi" Adrian alisema.

"Nimekuelewa Adrian, unafikiri kwanini Red butterfly kama inavyotupasa kuamini kuwa ni huyohuyo alienda katika kiwanda cha nguo cha Urafiki?" Daniel aliuliza.

"Kwa mujibu wa Meneja Christopher, Red butterfly alienda kuulizia kilekile nilichoenda kuulizia mimi. Na kwabahati nzuri ni mimi ndiye niliyefanikiwa kukipata. Sasa ninaamini katika safu hii ya uongozi kuna kitu ambacho Red butterfly alikuwa anakihitaji" Adrian alisema huku akitoa karatasi tano alizopewa na meneja Christopher na kumkabidhi Daniel.

"Uko vizuri sana Adrian. Kwakuwa waliouwawa wote walikuwa viongozi wa kiwanda cha Urafiki miaka hiyo bila shaka kwa kupitia kuangalia viongozi wa kipindi hiko tutapata jibu" Daniel Mwaseba alisema huku akiziangalia zile karatasi kwa umakini.

"Ona, ona Adrian, waliouwawa wote nane walikuwa viongozi wa mwaka 1955 hadi 1957" Daniel alisema kwa wahka mkubwa.

"Nimeliona hilo kaka Daniel ingawa wewe umechukua muda mfupi sana kugundua. Mwaka 1955 mpaka 1957 kiwanda cha Urafiki kilikuwa na viongozi kumi na tano katika kamati yake ya utendaji. Na nane kati ya hao wameuwawa kwa mkongojo wa Red butterfly. Kwa maana walibaki hai viongozi saba tu wa kipindi hiko. Lakini viongozi watano kati ya hao wameuwawa kwa magonjwa mbalimbali kabla ya tukio hili. So walio hai mpaka sasa ni viongozi watatu tu" Adrian alisema kwa kirefu.

"....ambao unapaswa kuwafatilia ili kujua kwanini viongozi wenzao wa kipindi hiko wanasakwa na Red butterfly" Daniel Mwaseba alidakia.

"Ndio kazi iliyopo mbele yangu baada ya kutoka hapa" Adrian alisema.

"Ila kuwa makini sana Adrian. Kwasasa Red butterfly anajua kwamba umemuwahi pale katika kiwanda cha Urafiki kwa kuchukua hizi nyaraka. Sasa atakusaka kwa kujua wewe ni mtu hatari kwake. Hakikisha kila unapoenda wakina Idd wapo nyuma yako wanakulinda, peaneni taarifa mara kwa mara. Unaenda hatua ya mwisho katika kufumbua fumbo la Red butterfly, kuwa makini sana katika hatua hii. Shirikiana na wenzako. Ushirikiano ni kila kitu katika misheni hatari kama hizi" Daniel Mwaseba alisema.

Waliendelea kuongea kama nusu saa kisha wakaagana. Waliongea pia kuhusu kupotea kwa Elizabeth Neville. Adrian alimwambia kuwa bado watu wa China wakiongozwa na Maxi Lee wanaendelea na uchunguzi wao. Mwishowe Adrian aliondoka akiwa na imani kubwa ya kwenda kufumbua fumbo la Red butterfly huku Daniel akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kwanini Red butterfly anafanya mauaji kwa viongozi wa kiwanda cha urafiki tu wa mwaka 1955 hadi 1957? na swali la wapi alipo mke wake Elizabeth Neville pia liliendelea kuganda katika kichwa cha Daniel Mwaseba...


Waliendelea kuongea kama nusu saa kisha wakaagana. Waliongea pia kuhusu kupotea kwa Elizabeth Neville. Adrian alimwambia kuwa bado watu wa China wakiongozwa na Maxi Lee wanaendelea na uchunguzi wao. Mwishowe Adrian aliondoka akiwa na imani kubwa ya kwenda kufumbua fumbo la Red butterfly huku Daniel akiwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kwanini Red butterfly anafanya mauaji kwa viongozi wa kiwanda cha urafiki tu wa mwaka 1955 hadi 1957? na swali la wapi alipo mke wake Elizabeth Neville pia liliendelea kuganda katika kichwa chake"

Tusome ya leo sasa...

Saa kumi kamili jioni Adrian Kaanan ilimkuta katika nyumba ya Fuga Kindo. Mmoja wa viongozi wa kiwanda cha nguo cha urafiki wa mwaka 1955 hadi mwaka 1957. Mzee Fuga Kindo alikuwa anaishi maeneo ya Tandika Foma ambako alijenga nyumba baada ya kustaafu. Adrian alifika Tandika na moja kwa moja alielekea katika nyumba ya mzee Fuga Kindo ambako alikuwa na umaarufu sana katika maeneo ya Tandika Foma.

Ilikuwa ni nyumba iliyobanana katikati ya nyumba nyingi sana. Adrian alifika hadi katika mlango wa nyumba ya mzee Fuga Kindo. Aligonga. Alipokewa na ukimya, hodi yake haikuitikiwa. Aligonga tena, bado ilikuwa kimya. Aligonga tena na tena. Bado hali ilikuwa ileile ukimya wa kimya. Akaongea katika kifaa maalum alichovaa ili kuwasiliana kina Idd.

"Hapa kimya kabisa. Sijui huyu mzee katoka?"

"Sidhani. Tafuta mjumbe wa mtaa ili tupate ruhsa ya kuvunja mlango na kuingia ndani. Inawezekana Red butterfly katuwahi tena" Idd alisema.

"Sawa Soldier" Adrian akajibu.

Dakika kumi na nane baadae walikuwa katika mlango wa mzee Kindo wakiwa na mjumbe wa mtaa, shahidi mmoja pamoja na fundi seremala. Fundi seremala alitumia dakika zisozozidi tano kuvunja mlango ule. Mlango haukuweza kuhimili ufundi wa fundi yule. Sasa walikuwa ndani ya nyumba ya mzee Kindo. Walitafuta huku wakiita kwa dakika kadhaa, bado kulikuwa kimya kama awali. Mzee Kindo hakuwepo.

"Itakuwa kaenda wapi huyu mzee?" Adrian akaipata sauti.

"Mzee Kindo amekuwa akilala hapa kitandani kwa miaka kumi sasa. Amepooza hivyo hawezi kutembea. Suala la kutokuwepo leo ni la ajabu sana" Mjumbe alijibu.

"Au ndugu zake wamekuja kumchukua?" Adrian aliuliza tena.

"Sidhani. Mzee ana ndugu mmoja tu ambaye alikuwa anakuja kumsaidia mara kwa mara. Huwa anamletea vitu hapa na kuondoka" Yule jirani akasema.

"Yupoje huyo mwanamke?" Adrian aliuliza.

"Ni mwanamke mrefu mweupe. Nywele zake amezifunga kwa nyuma. Mara nyingi huja na pikipiki. Huja mara kwa mara hapa na kumwachia pesa nyingi sana mzee Kindo" Yule jirani akajibu.

" Mliwahi kumuuliza mzee Kindo ana uhusiano gani na huyo mwanamke?" Adrian aliuliza.

"Mzee Kindo hakutaka kabisa kumzungumzia yule mwanamke. Ilikuwa ukitaka kumuuzi muulize kuhusu yule mwanamke" Yule jirani akasema.

"Red butterfly. Sifa zote ni za yule mwendawazimu" Adrian aliwaza. Huku moyoni akiamini kwamba walikuwa wamezidiwa tena ujanja na Red butterfly.

"Sasa kwanini viongozi wengine wa kiwanda cha nguo cha urafiki wa mwaka 1955 wamewauwa lakini mzee Kindo hajamuuwa? Na zaidi amekuwa anamuhudumia?" Adrian alijiuliza lakini majibu yalikuwa mbali sana. Ulikuwa utata mwengine ndani ya fumbo la yule mwanamke wa ajabu. Mwanamke anayeitwa Red butterfly..

Baada ya maongezi na wale watu Adrian aliondoka huku wakipeana namba za simu. Adrian aliondoka kichwa chini, alikuwa na mawazo yasiyo na kifani. Hii kesi ilikuwa ngumu sana kwake.

"Hallo Adrian" Kile kifaa cha masikioni kiliita.

"Eeeh Idd, mambo magumu sana. Sasa wamebaki watu watatu tu wa kuweza kutufumbulia fumbo hili. Mzee Togo Lunyanda na Mzee Kondo Habibu. Wakati sasa tukiwasaka hao wazee bila shaka na Red butterfly naye anawasaka kwa udi na uvumba. Sasa tujigawe, wewe na askari wawili nendeni kwa mzee Togo Lunyanda kule Mabibo na mimi ninaenda kwa mzee Kondo huko Gongo la mboto. Naomba muende kwa haraka huku mkiwa makini. Hawa wazee wawili ni muhimu sana, tukiwapoteza yaani tumepoteza kila kitu" Adrian alisema.

"Sawa Adrian nimekuelewa. Tuwe tunawasiliana basi mara kwa mara tujue tumefikia wapi?"

Pikipiki tatu zikajigawa. Idd na askari wawili walielekea Mabibo kwa mzee Togo Lunyanda huku Adrian na askari wawili walielekea Gongo la mboto kwa mzee Kondo Habib.

Idd na wenzake ndio walikuwa wakwanza kufika Mabibo nyumbani kwa kwa mzee Togo Lunyanda. Alipofika maeneo ya chuo cha NIT alisimamisha pikipiki yake na kumuuliza kijana mmoja aliyekuwa anachoma mahindi barabarani. Alielekezwa. Moja kwa moja alienda nyumbani kwa mzee Togo Lunyanda huku nyuma yake akifuatwa na pikipiki za askari wawili kwa siri.

Ilimchukua dakika moja tu kufika. Hakukuwa mbali sana. Ilikuwa nyumba ya wastani iliyojitenga. Adrian alipiga hodi. Aliitikiwa.

Mlango ulifunguliwa, alitoka mama mmoja wa makamo.

"Habari yako" Alisalimu Adrian.

"Nzuri mwanangu wangu. Karibu sana" Yule mama alijibu.

"Samahani mama nilikuwa namuulizia mzee Togo Lunyanda, nimemkuta?" Adrian alisema.

"Mzee amelazwa Muhimbili wiki sasa ana tatizo katika njia ya mkojo" Yule mama alisema.

"Yupo katika wodi gani? Nina shida naye muhimu sana" Adrian alisema.

"Yupo katika wodi ya Mwaisela" Yule mama alijibu.

Adrian aliaga na kwenda kwenye pikipiki yake. Kwa kasi alikuwa anaelekea katika hospitali ya Muhimbili kuonana na Mzee Tondo. Mtu muhimu sana katika kufumbua fumbo la Red butterfly.

Njiani Adrian aliwasiliana na kina Idd.

"Hallo Idd?" Aliita.

"Idd unanisikia?" Ilikuwa kimya.

"Idd, Idd Adrian hapa unanisikia?" Adrian aliita. Bado ilikuwa kimya.

"Mbona Idd hapatikani. Au kutakuwa na tatizo la mtandao" Adrian aliwaza. Kipindi hiko alikuwa Magomeni Mwembechai akielekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Dakika kumi tu baadae alikuwa nje ya geti ya hospitali ya mkononi. Ndipo simu yake ya mkononi iliita. Aliitoa simu yake mfukoni na kuipokea. Ilikuwa ni simu kutoka kwa IGP John Rondo. Moyo wa Adrian ukastuka, akajua kuna kitu.

"Haloo mkuu, habari yako" Adrian alisalimu.

"Nzuri Adrian, upo salama kweli?" IGP John Rondo aliuliza kwa sauti yenye wasiwasi.

"Nipo salama, nipo Muhimbili hapa nikiifatilia ile kesi" Adrian alisema.

IGP alishusha pumzi ndefu na kuuliza "Kina nani walienda Gongo la mtoto?"

"Idd, Francis na Kennedy" Adrian alijibu.

"Nimepokea taarifa hapa. Kuna mzee mmoja ameuwawa na askari wote watatu wamejeruhiwa na risasi dakika tano zilizopita" IGP John Rondo alisema.

Nasema hivi mzee mmoja ameuwawa na askari wote wamejeruhiwa huko Gongo la mboto. Kuna shambulio lililodumu kwa dakika saba. Aliyewashambulia amefanikiwa kukimbia huku wakina Idd wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana!!" IGP John Rondo alisema.

"Red butterfly.." Adrian alisema kwa sauti ndogo iliyosikiwa na IGP John Rondo.

"Red butterfly yupo Gongo la mboto?" IGP John Rondo.

Adrian alimueleza kila kitu IGP John Rondo ilivyokuwa mpaka wakaenda kule Tandika Foma, na jinsi walivyojigawa ili kumpata Red butterfly.

"Ngoja nikuache Adrian. Nenda haraka kaongee na huyo mzee. Kuwa makini sana Adrian. Kwa vyovyote Red butterfly yupo njiani anakuja huko. Naleta askari hapo hospitali ili akija tu uwe ndo mwisho wake!" Adrian aliisikia sauti ya hasira kutoka kwa John Rondo.

Simu ikakatwa.

Harakaharaka Adrian aliingia ndani ya hospitali kwenda kuonana na Mzee Tondo Lunyanda. Alienda moja kwa moja katika wodi ya Mwaisela. Mlangoni alikutana na watu wakiutoa nje mwili wa mtu. Hakuwa na haja ya kuambiwa kwamba yule alikuwa tayari amekufa. Adrian alikuwa anaomba ile maiti isiwe ya mzee Tondo Lunyanda. Alimvuta nesi mmoja aliyekuwa anawafata nyuma wale manesi wengine waliobeba maiti. Kwa pupa aliuliza.

"Mzee Tondo Lunyanda yupo humu wodini?"

"Loh mzee amefariki dakika mbili zilizopita, ndio huyo tunampeleka monchwari.." Adrian hakusikia maneno ya mbele ya yule nesi. Aliona kama kaibeba dunia nzima peke yake. Sehemu pekee aliyokuwa anaitegemea sasa haikuwepo tena. Fumbo la red butterfly liliendelea kuwa fumbo la siri!

Mara simu yake iliita, alikuwa ni IGP John Rondo. Akaipokea.

"Mzee Tondo amefariki" Ndio ilikuwa kauli ya kwanza ya Adrian.

"Unasemaje Adrian?" IGP John Rondo aliuliza.

"Mzee amefariki. Nikiwa naingia wodini hapa mlangoni niliona manesi wakitoa maiti ndani ya wodi ya Mwaisela. Nilimuita nesi mmoja na kumuuliza. Ni huyo ndio aliyenambia kwamba mzee Tondo alikuwa amefariki dakika chache zilizopita" Adrian alisema.

"Asalaleeee tumepoteza tena ushahidi!" IGP John Rondo alisema simuni.

"Sahivi ninataka kurudi Mabibo nikaongee na yule mjane wa marehemu labda nitapata chochote. Maana watu wawili muhimu wameuwawa huku mmoja akipotea katika mazingira ya kutatanisha" Adrian alisema.

"Safi Adrian fanya hivyo. Gari moja ya askari itakuwa nyuma yako popote utapokwenda" IGP John Rondo alisema.

"Ahsante sana. Nashukuru sana" Adrian alisema.

Akatoka nje, akachukua pikipiki yake na kuelekea Mabibo. Ndani ya dakika kumi na mbili alikuwa mbele ya nyumba ya mzee Tondo Lunyanda. Alishuka kwenye pikipiki na kwenda kugonga hodi.

"Karibu" Alikaribishwa. Ilikuwa sauti ileile ya awali.

Baada kama ya sekunde thelathini mlango ulifunguliwa. Alitoka yule mwanamke aliyekuwa anaongea nae awali ambaye alikuwa mke wa mzee Tondo Lunyanda. Bila shaka hakuwa taarifa na kifo cha mumewe.

"Samahani sana mama, nimerudi tena" Adrian alisema.

"Karibu sana mwanangu"

"Safari hii naomba tukae ndani nina maongezi marefu kidogo na wewe" Adrian alisema.

Adrian na yule mama waliingia ndani ya nyumba. Walikaa kwenye sebule dhaifu iliyokuwa na samani zilizochakaa.

"Samahani tena mama yangu kwa kukupotezea muda wako" Adrian alianza kusema.

"Bila samahani mwanangu. Jisikie huru" Yule mama aliongea kwa sauti ya upole.

"Kwa majina naitwa Adrian, ni askari wa jeshi la Polisi. Katika majukumu yangu ya kazi nimepewa kazi ya kuchunguza kifo cha waziri Elisha Ngwena na watu wengine saba. Katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wanauwawa ni wale waliokuwa viongozi wa kiwanda cha nguo cha urafiki mwaka 1955 hadi mwaka 1957. Ambapo mumeo pia alikuwa kiongozi kipindi hiko. Katika uchunguzi wangu pia nimegundua uhusika wa Mwanamke aitwaye Red butterfly katika mauaji hayo. Sasa nilikuja kwako ili niongee na mumeo labda anajua chochote juu ya vyanzo vya vifo hivyo. Kwa bahati mbaya nimeenda hospitali nimemkuta mzee hayupo tayari kuongea kutokana na maradhi yake, ndipo nimekuja kwako kukuuliza labda unajua chochote sababu ya vifo hivyo" Adrian alieleza kwa kirefu.

"Nimekuelewa mwanangu ila kuna sehemu moja sijakuelewa. Kuna sehemu kuna uhusika wa Mwanamke sijui anaitwa nani?"

"Red butterfly" Adrian akadakia.

"Hapo ndio sijalielewa hilo jina lina maana gani?" Yule mwanamke aliuliza.

"Red butterfly ni kwa kiingereza kwa kiswahili ni kipepeo mwekundu, ame...." Adrian hakumaliza kuelezea.

"Kipepeo mwekundu!! Muuaji ni kipep..." Yule mwanamke hakulirudia tena hilo neno.

Katikati ya paji la uso zilikuwa zinamwagika damu!! Bila shaka bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti ilikuwa imefanya kazi yake sehemu fulani. Yule mama alilalia lile kochi kuukuu kwa shingo upande, mdomo ukiwa wazi ukitaka kuelezea chochote kuhusu kipepeo mwekundu. Macho alikuwa ameyatoa akimwangalia Adrian. Hakukuwa na haja ya daktari yule mwanamke hakuwa katika sayari hii. Alikufa siku sawa na aliyokufa mume wake wakipishana dakika chache sana.

Adrian alikuwa amerukia nyuma ya kochi na bastola yake mkononi. Alikuwa anaangalia kwa umakini madirisha yote mawili ni wapi ilipopenya ile risasi. Bila shaka kutoka katika bastola ya Red butterfly...

Mambo yamekuwa magumu zaidi, je Adrian atafanikiwa kumnasa Red butterfly? Na je wale askari walio kule nje hawajamuona Red butterfly? Majibu yote yapo ndani ya simulizi hii ya aina yake...


Adrian alikuwa amerukia nyuma ya kochi na bastola yake mkononi. Alikuwa anaangalia kwa umakini madirisha yote mawili ni wapi ilipopenya ile risasi. Bila shaka kutoka katika mkono wa Red butterfly.

Ndani kulikuwa kimya. Adrian akanyanyuka kidogo kule nyuma ya kochi na kuangazaangaza, kulikuwa kimya vilevile. Akanyata taratibu katika dirisha ambalo alikuwa na uhakika mpigaji wa risasi ile ndilo alilolitumia, alifika, akachungulia kwa nje pembeni kabisa mwa dirisha lile, hakukuwa na mtu, ingawa aliliona tundu dogo ilipopenya ile risasi.ITAENDELEA