Saturday, 4 January 2020

MAHABA NIUE

MAHABA NIUE
MAHABA NIUE

SIMULIZI FUPI - MAHABA NIUE

Ni jioni yapata saa kumi na mbili kijana mtanashati,mkarimu,mwenye mvuto wa sura hata mwili kwani amejijenga mwili mithiri ya yule mwanamieleka wa marekani(wwe)john cena,si mwingine ni Abdul ramadhani kijana wa kindamba aliyekua anaishi magomeni pamoja na wazazi wake,alikua anaongea na mpenzi wake aliyempenda kwa dhati hata akagombana na familia yake.


Si mwingine ni Latifa binti wa kingoni mwenye haiba ya kike kwani hata anapopita mbele ya wanaume rijali basi lazma watasimamwa na maungo yao ya siri.

Binti yule alikua anasoma Zanaki sekondali shule ya wasichana iliyopo katikati ya jiji la dar.Abduli alikua ameambiwa na rafiki yake anayefanya nae mazoezi ya kickboxing Fadhili kua Latifa anamahusiano ya kimapenzi na kaka mmoja wa makamo kama miaka 40 kitu ambacho hakikua na ukweli hata kidogo.

Siku hiyo abdul aliamua kunywa pombe aina ya banana wine kinywaji ambacho kinapendwa na vijana wengi dar hata arusha kutokana na kutokua ghali,alipotoka kijiweni akamtafuta latifa ili amtolee maneno machafu ya kujiamini."toka na nisikuone maishani mwangu" ni maneno aliyotamka Abdul kwa latifa."nisamehe mpenzi wangu,acha kusikiliza maneno ya watu wasiopenda mapenzi yetu"latifa alijibu.

Ilikua asubuhi na mapema abduli anaamka kujiandaa kwenda shule,alikua anasoma shule ya sekondali alharamain islamic alikua mwaka wa mwisho kuhitimu masomo yake ya kidato cha nne,asubuhi ile ilikua nzuri kwa abduli lakini siyo latifa aliyekua na maumivu ya kusalitiwa na mtu aliyempenda kwa dhati."

Eeh mungu wangu sina cha kupoteza ni bora nife"ni maneno aliyoyasema latifa akiwa ameshika sumu ya panya tayari kuinywa.ghafla anatokea mama yake lakini tayari alikwisha chelewa kwani latifa alikua amesha kunywa ile sumu,haraka wakamuaisha hospitali ya karibu akapewa dripu ya maji na kuondoa ile sumu."

Mungu alikua pamoja nae,yuko hai"ni maneno ya nesi wa zamu akimwambia mama yake baada ya latifa kufumbua macho."

Nitamchukia yule kijana milele"ni maneno makali yaliyomtoka mama latifa akidhihilisha chuki kali juu ya kijana abdul.jioni ya siku ile abduli alikua akijivinjali na mrembo aitwae dorothea wengi walimuita dora,mrembo wa kidigo mrefu mwenye kiuno cha dondola na kishepu cha uchokoz pia alikua ni dada wa nikolas ambaye ni rafiki wa karibu wa abdul,amakweli abdul alikua hachagui wala habagui atakaye mzika hamjui.

Alikua ni mpenzi mwingine wa abdul na siku hiyo walikua wakipeana mahaba mazito ndani ya uwanja wa sita kwa sita"ooh ooh aah aass hapo hapo baby"ni miguno iliyosikika chumbani kwa abdul,dola akiwa analalamika vilio vya mahaba.

Hakika abdul alikua anajua kuwafikisha wanawake kileleni hakuna mwana mke aliyepita mikononi mwake bila kupagawa na mapenzi ya abdul."

Niache nimuoneshe mshenzi mkubwa huyu,gumegume lililomshinda mtume"ni maneno aliyoyatoa binti mmoja ajulikanae kama Siyawezi wakati anapigana na jirani yake,pia ni rafiki yake ajulikanae kwa jina la mwanaisha kisa kikiwa ni kijana abdul."waacheni waoneshane malaya hao"yalisikika mayoe kutoka kwa vijana wa kijiweni waliokuwepo maeneo hayo.

Ni kama wana karate au boxing pale siyawezi aliporusha ngumi aina ya right cross na mwanaisha kuinama ngumi ikapita kisha nae kutoa pigo kali lililo mkuta siyawezi kidevuni na kumtupa kando ilikua ni uppercut."ambakati chembe kidevu lazima ukae!!!"

Alitamka kijana mmoja aliyefurahia pigo lile lililo mfanya siyawezi agalegale pale chini mithili ya nyoka ajivuae magamba.wakati hayo yanatokea ilikua ni miezi minne tangu abdul afanye mtihani wake wa taifa kidati cha nne,na latifa akiendelea kuomba radhi kwa mpenzi wake warudiane kitu ambacho kwa kijana kama abdul alikua anatwanga maji kwenye kinu,kwani abduli alikua na hulka za kilevi akilala na mwanamke leo hakuitaji tena(playboy).

abdul hakufaulu mitihani yake kitu kilichomfanya arudie mitihani yake ili aweze kuendelea na masomo ya juu kama ndoto zake zilivyo kuwa awe mwanasheria,kweli hakukata tamaa aliendelea na mapambano akirudia masomo yake wakati huo mama yake abdul Bi asma maarufu kama ticha au MC alitumia muda wake kusali akimuombea mwanae aweze kufaulu mitihani iliyo mbele yake.ilikua jioni ya alhamisi abdul alikua katika moja ya misele yake safari hii alikua akimuwinda binti aitwae shani binti mzuri wa sura hata umbo bila kusahau tabia,binti ambae abdul aliona ndio binti anaestahili kupewa heshima ya uchumba kwake,hakika kwa binti huyu abdul hakua na chembe ya kumchezea alimpenda kiukweli na alitamani siku moja awe mkewe.mara zote abdul anapojalibu kutupia mistali yake kwa shani iligonga mwamba hivyo ilimpa abdul wakati mgumu sana kwani moyoni kwake shani alikua ameenea hata ukimkata abdul damu yake itajiandika shani.

Kipindi chote hicho latifa aliendelea kumuomba abdul warudiane kwa ghalama yoyote ile lakini kwa abdul wembe ulikua ni ule ule haitaji kua naye,ni wakati huohuo abdul alikua tayari ameshaanzisha mahusiano ya kimapenzi na rafiki wa latifa aitwae Pinato mtoto wa kinyaluanda mwenye shepu namba nane makalio kama anachambia hamila.

Wengi walizoea kumuita pina kifupi cha jina lake,baada ya shani kumtema abdul moja kwa moja abdul aliamua kutuliza machungu yake kwa binti mwingine aitwaye maryam binti wa kitanga ambae kwa muda mrefu alikua akimpenda abdul lakini hakuwahi kumwambia ila baada ya abdul kumtamkia kua anampenda maryam hakujivunga mara moja alimkubalia abdul kwa moyo mmoja,lakini kwa abdul ilikua ni kujalibisha makali ya kisu chake kwanini moshi alimkataa.


Mapenzi ya abdul na maryam yalinoga kama tembele lililoungwa kwa nyanya masalo,ndimu na pilipili hakika hata abdul alimsahau shani na kujikuta amenata kwa maryam.

amakweli ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu kumbe kipindi chote hicho maryam alikua na mahusiano na kijana mchezaji wa mpira wa miguu aitwae tiga na abduli alipogundua hilo haraka aliachana na maryam,abdul hakupenda kuumizwa kama anavyo waumiza wanawake zake.siku moja kama zali kwa mentali shani akaingia kwenye mikono ya abdul baada ya kumkatalia kwa muda kwasababu yeye alikua amechumbiwa na kijana mmoja ambaye waliachana baada ya yule kijana kulazimisha kukutana kimwili na shani kitu ambacho shani aliazimia kukifanya baada ya ndoa.Abdul akang'oa mchuma na shani kujikuta amedondoka katika mikono ya abdul,lahaula!! akazama kwenye dimbwi la mahaba ya abdul kama kawaida ya abdul ukiingia mikononi mwake hutoki,

Ilikua ni furaha kubwa kwa abdul lakini shani hakujua kilichopo mbele yake. Abdul alifaulu masomo aliyokua anarudia na kumuwezesha kuendelea na kidato cha tano,kwelishule alipata pafect vision iliyopo maeneo ya ubungo,kama kawaida ya abdul alianzisha mahusiano ya kimapenzi na binti aliyekua nae darasa moja yeye ni monita na yule binti ni monitress.

Mwanzoni abdul hakuonesha hisia za kimapenzi kwa yule binti kitu kilichomfanya faith au imani maarufu kama imma kukazana na kumtongoza abdul pamoja na kumuhonga pesa na vito vya thamani hatimae Abdul mpenda vya dezo akaingia laini.

Wakati abdul anaingia kidato cha sita alimwambia mpenzi wake nyongo mkalia ini shani kwamba wawe mbalimbali ili abdul aweze kujiandaa vizuri na mitihani yake ya mwisho,loh!! makubwa yakamfika pale imma alipomfanya abdul ajutie maisha yake na ujinga wake.

ni baada ya imma kulazimisha kulala nyumbani kwa abdul kitu kilichopelekea kwao kumtafuta,hata aliporudi kwao ilimlazimu aambatane na mama na baba yake pamoja na polisi mpaka nyumbani kwa abdul.

Ilikua jumanne usiku abdul akijiandaa na mitihani ya kesho asubui language two na g/s ghafla mlango ukagongwa abdul alipofungua uso kwa uso na mtutu wa bunduki"ndio huyu"alisema askali aliyebeba silaha aina ya smg iliyokatwa kitako"ndio huyo"ni sauti iliyopenya moja kwa moja masikioni mwa abdul na kujikuta akihamaki"imma!!"abdul alihamaki lakini alikua ameshachelewa polisi wale nane walimchukua pamoja na mama yake abdul moja kwa moja kituo cha polisi magomeni na wote abdul na mama yake wakaswekwa ndani.

Ally rafiki mkubwa wa abdul pia ni general secretaly pale pafect vision alishangaa kutomuona abdul katika mitihani ile hususani language ambayo ndiyo abdul alikua akifanya vizuri pale shuleni.shani akihangaika nini kimemkuta mpenzi wake,ndipo walimwengu walipo mueka wazi kwamba abdul na mama yake wako polisi kutokana na abdul kukutwa chumbani akifanya mapenzi na binti aliyekua ni mwanafunzi.


Moyo ukampaa!!hakuweza kuvumilia tena akajikuta analia huku akilalamika kwamba abdul alimwambia awe mbali nae ili ajiandae na masomo kumbe alitaka uhuru wa kufanya uchafu wake binti alilia akijutia ahadi zote alizopewa na abdul zilikua ni uwongo tena uzandiki mkubwa.

Mchana wa siku hiyo abdul na mama yake walipata dhamana na mwisho ile kesi ikaisha kwa makubaliano ya kulipa faini kwa ile familia ya imma shilingi laki tano ili kesi isifike mbali,kumbe imma na mama yake ule ulikua ndio mchezo wao pale mjini.

Aibu ilimtawala abdul si nyumbani wala shuleni na kila alipomuona imma moyo wake ulimpasuka vibaya kiasi cha kutaka kumrarua,na abdul aliahidi kulipa kisasi siku yoyote katika maisha yake.

Hapo abdul kama simba aliyekosa nyama ilimbidi ale majani,akakata shauri baada ya kugundua kwamba latifa hakuwahi kumsaliti aliamua kumwangukia na kuomba radhi.hakika muungwana akivukwa nguo huchutama,pamoja na hayo yote lakini latifa tayari alikua na mahusiano mapya na kijana mwingine christofa maarufu kama criss kijana wa kinyamwezi mwenye weredi wa kiume na tayari alishamchumbia.


Abdul akajikuta katika maumivu mengine,ama kweli mungu hamtupi mja wake baada ya miaka miwili ya maumivu,majonzi na majuto akapewa nafasi nyingine.

Kwa mapenzi aliyokua nayo shani aliweza kumsamehe abdul na wakarudiana na kuyatupilia mbali yaliyopita,hatimae abdul akamaliza kidato cha sita kwa alama nzuri(division two),yeye pamoja na rafiki yake Ally na imma kutokana na tabia yake ya kutumia mwili wake kama njia ya kujiingizia kipato alifeli na kuambulia mimba ya muuza chips pale ubungo.hakika kama mungu amekuandikia mafanikio basi hata iweje utajikuta kwenye mafanikio,kwani abdul alidumu na shani hata wakapata mtoto wa kike waliyemuita Precious!!


********MWISHO*********